1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano kuhusu bajeti ya Ulaya waanza Brussels

Josephat Nyiro Charo22 Novemba 2012

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanaanza mkutano wa siku mbili leo mjini Brussels kujadili bajeti ya mwaka 2014-2020. Kunatarajiwa malumbano makali kwenye, huku viongozi wakiwa na misimamo tofauti kuhusu matumizi ya fedha.

https://p.dw.com/p/16oGY
Greece's Prime Minister Antonis Samaras arrives at the EU council headquarters for an European Union leaders summit discussing the European Union's long-term budget in Brussels November 22, 2012. EU heads of state and governments will need to agree a first-ever cut in the bloc's long-term spending plans if they are to clinch a deal at a summit starting on Thursday, with the drive for austerity likely to trump all other concerns. REUTERS/Francois Lenoir (BELGIUM - Tags: POLITICS BUSINESS)
EU-Gipfel in Brüssel HaushaltsplanungenPicha: Reuters

Mkutano huo unafanyika huku viongozi wakikabiliwa na shinikizo la kuepukana na makosa yaliyofanywa awali, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa barabara kubwa kubwa ambazo hazina magari mengi, viwanja vya ndege ambavyo ni nadra kutumiwa kwa usafiri wa ndege na reli za treni za kwenda kasi zinazobeba abiria wachache. Viongozi wanakabiliwa na changamoto ya kulipa fedha zilizotumika katika miradi hiyo.

Kunatarajiwa kuwa na kibarua kigumu kufikia makubaliano ya bajeti ya Umoja wa Ulaya ya mwaka 2014-2020 katika mkutano huo. Changamoto nyingine kubwa itakuwa kujiepusha na majaribu ya kutenga mabilioni ya euro kwa ajili ya miradi ambayo baadaye inakuwa ni kumbukumbu ya hasara tupu.

Baustelle EU. Baustellenschild vor einer Baustelle am Rond point Schuman, Brüssel. Im Hintergrund das Gebäude des Europäischen Rates, Ratsgebäude Justus Lipsius, Aufgenommen am 22.11.2012 in Brüssel. Foto: Bernd Riegert, DW
Eneo la mkutano BrusselsPicha: DW

Fedha zinazotumika kwa ajili ya ujenzi wa barabara, daraja na miundombinu mingine katika maeneo masikini kabisa ya Umoja wa Ulaya zinajumuisha asilimia 33 ya bajeti ya thamani ya euro trilioni 1 kwa kipindi cha miaka saba ijayo. Kiwango hiki kinakariba fedha zilizotengwa kwa ajili ya kilimo.

Tofauti kubwa ya maoni

Nchi kadhaa zimeapa kutumia kura yao ya veto kukwamisha bajeti iliyopendekezwa. Nchi zinazochangia kiwango kikubwa cha fedha zinataka bajeti hiyo ipunguzwe kufikia bilioni 100 zikisema haiingii akilini kuongeza matumizi katika Umoja wa Ulaya wakati nchi za Ulaya zikifunga mkaja.

Ujerumani inaamini kushindwa kwa viongozi wa Ulaya kukamilisha bajeti hiyo halitakuwa jambo kubwa la kutia wasiwasi. Duru za serikali ya Ujerumani zinasema bado kuna muda na kwamba kama miezi kadhaa itahitajika ili kutolewe maoni na uratibu wa kisiasa ufanyike katika miji mikuu ya Ulaya, basi hautakuwa mwisho wa dunia.

Waziri mkuu wa Luxembourg, Jean-Claude Juncker, ambaye anaongoza jopo la mawaziri wa fedha wa kundi la nchi zinazotumia sarafu ya Euro, ameonya kuhusu mazungumzo magumu katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya mjini Brussels. Juncker amesema misimamo inatofautiana mno na haitokuwa rahisi kufikia mapatano kwa haraka.

Luxembourg's Prime Minister Jean-Claude Juncker leaves the EU council headquarters for an European Union leaders summit discussing the European Union's long-term budget in Brussels November 22, 2012. EU heads of state and governments will need to agree a first-ever cut in the bloc's long-term spending plans if they are to clinch a deal at a summit starting on Thursday, with the drive for austerity likely to trump all other concerns. REUTERS/Yves Herman (BELGIUM - Tags: POLITICS BUSINESS)
Jean-Claude JunckerPicha: Reuters

Fedha za Umoja wa Ulaya zimeleta manufaa makubwa kwa watu masikini katika mataifa ambayo hayajaendelea sana Ulaya na kwingineko duniani. Kwa mfano zimesifiwa kwa kuisadia Poland kuepuka kutumbukia katika mdororo wa kiuchumi wakati wa mgogoro wa sasa wa uchumi na kwa kuyaokoa maisha ya wengi kupitia misaada ya kigeni na kusaidia utafiti wa kitabibu.

Viongozi kumwaga cheche

Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron, leo ameapa kupigania bajeti itakayodhihirisha hatua za kubana matumizi zinazofanywa kitaifa kwa masilahi ya walipa kodi wa Uingereza na Ulaya nzima kwa ujumla.

Britain's Prime Minister David Cameron arrives at the EU council headquarters for a European Union leaders summit discussing the European Union's long-term budget in Brussels November 22, 2012. EU heads of state and governments will need to agree on a first-ever cut in the bloc's long-term spending plans if they are to clinch a deal at the summit starting on Thursday, with the drive for austerity likely to trump all other concerns. REUTERS/Yves Herman (BELGIUM - Tags: POLITICS BUSINESS)
Waziri mkuu wa Uingereza, David CameronPicha: Reuters

Akizungumza muda mfupi baada ya kuwasili Brussels, Cameron amesema haridhiki kabisa na pendekezo la bajeti wakati huu wanapopitisha maamuzi magumu kuhusu matumizi ya fedha za umma. Amesema litakuwa kosa kubwa kuwepo na pendekezo la kuongeza matumizi katika bajeti ya Ulaya.

Kwa upande mwingine, waziri mkuu wa Ubelgiji, Elio Di Rupo, ameonya leo kwamba kupunguza kwa kiwango kikubwa matumizi katika Umoja wa Ulaya litakuwa kosa kubwa. Amewaambia waandishi wa habari alipowasili mjini Brussels kuwa, "Lazima tuwe na bajeti yenye malengo makubwa. Kwa sasa tunahitaji uwezo wa kifedha kuliko wakati mwingine wowote, ili tuweze kusambaza upya, tuwe na sera mpya - yaani sera za viwanda."

Di Rupo amesema atapigania fedha za kutosha kwa ajili ya kilimo na maeneo masikini kabisa ya Ulaya, ikiwa ni pamoja na jimbo la nchi yake la Limburg, ambalo lilipatwa na mshangao mkubwa mwezi uliopita kwa taarifa za kufungwa kiwanda cha kutengeneza magari cha kampuni ya Ford. Hakuondoa uwezekano wa kutumia kura ya turufu ikihitajika.

Mwandishi: Hasselbach, Christoph/Josephat Charo

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman