1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano mkuu wa chama cha Demokratik ,Denver Colorado.

Mtullya, Abdu Said26 Agosti 2008

Mkutano mkuu wa chama cha Demokratik umeanza leo mjini Denver.

https://p.dw.com/p/F4mA

DENVER:

Wanachama wa chama cha Demokratik wameanza mkutano wao mkuu wa siku nne mjini Denver Colorado, ambapo wanatarajiwa kumpitisha rasmi Barack Obama kukiwakilisha chama hicho katika uchaguzi wa rais nchini Marekani.

Hii ni mara ya kwanza kwa chama cha Demokratik kumchagua mjumbe mwenye asili ya kiafrika kugombea urais wa Marekani.Uchaguzi huo utafanyika mwezi novemba.

Wajumbe alfu tano wanahudhuria mkutano huo ambapo viongozi wa chama wanatarajiwa kuwahamasisha wafuasi wa seneta Hillary Clinton wamwuunge mkono Barack Obama.

Seneta Clinton alieshindwa na Obama katika kugombea nafasi ya kukiwakilisha chama cha Demokratik anatarajiwa kuhutubia kwenye mkutano huo leo.

Akihutubia kwenye mkutano huo mke wa seneta Obama, Michelle aliwaambia wajumbe kuwa mume wake atakuwa rais mzuri sana.Amesema dunia inahitaji mabadiliko na kwamba chama cha Demokratik kina dhima katika kupigania dunia hiyo.

Wakati huo huo seneta mahiri Edward Kennedy alitokea kwenye mkutano huo licha ya afya yake kuwa mbaya.Seneta Kennedy amesema ameenda kusimama pamoja na wanachama wengine ili kurejesha mustakabal wa Amerika kwa kumchagua Barack Obama kukiwakilisha chama cha Demokratik katika uchaguzi wa rais.