1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa ASEM kati ya Asia na Umoja wa Ulaya

30 Mei 2007

Mada nyengine iliohaririwa na wahariri wa magazeti ya Ujerumani ilikua alama za kuzitambulisha bidhaa.

https://p.dw.com/p/CHSq

Mkutano wa mawaziri wa nje wa Umoja wa Ulaya na mawaziri wenzao 16 kutoka nchi za Asia –ASEM-kwa ufup I na pendekezo la la viwanda kuwa bidhaa zaq vyakula madukani ziwe na vitambulisho wazi- ndizo mada 2 kuu zilizotia fora leo katika safu za wahariri wa magazeti ya Ujerumani.

Gazeti la MITTELBAYERISCHE ZEITUNG laandika:

“ Ikiwa mkutano uliomalizika jana wa ASEM kati ya UU na nchi za Asia ni mtihani wa kwanza kwa kikao kijacho cha kundi la dola kuu 8 za kiviwanda G-8,basi haukufanikiwa.Hakuna yeyote mwenye hamu na matokeo.

Ghasia zilizozuka usiku wa kuamkia jumatatu ziligubika picha nzima .Kwa jicho hilo mkutano wa kilele wa Heiligendamm utakua kiini macho tu ambamo wanasiasa na waandamanaji watakuwa wametengana zaidi kuliko na ua wa senyenge wa kuwalinda.

Ikiwa haitafanikiwa mada muhimu ya mkutano huo kuiweka usoni kabisa na kuipatia ufunbuzi,basi kikao cha Heiligendamm kitakua kazi ya bure.”

Gazeti la Nüremberger Zeitung limejishughulisha mno na msimamo wa China juu ya uchafuzi wa mazingira.Laandika:

China ikipaza hewani moshi wa kiasi cha tani bilioni 5 kila mwaka tayari ni dola la pili nyuma ya Marekani katika orodha ya wachafuzi wakubwa wa hali ya hewa.China imeitikia shingo upande kubeba jukumu la dola za kiviwanda katika kuchafua mazingira kwa kupaza moshi kutoka viwandani.”

Mod. Ama gazeti la FRANKFURTER ALLGEMEINE ZEITUNG linakosoa vikali maswali nyeti yanayozushwa na wapinzani wa kundi la G-8.Lasema:

“Hata ukielewa vipi malalamiko juu ya mkutano wa kilele wa kundi la G-8 huko Heiligendamm,malalamiko yanayotolewa nayo pia sio hayapingani.Kwa upande mmoja kundi hilo la G-8 pamoja na Russia linatuhumiwa kuwa linajitokeza kama ndio serikali ya dunia hii na kwa upande wapili linatakiwa kutimiza madai ambayo yaweza tu kutekelezwa na dola zenye nguvu kama hizo za G-8:mfano kupiga vita umasikini na ,vita na magonjwa barani Afrika.

Likitugeuzia mada ,gazeti la Stuttgarter Nachrichten lazungumzia dai la viwanda vya Ujerumani kutaka bidhaa madukani na hasa za vyakula kuwa na vitambulisho wazi ili kujulikana asili yake na zimetemngezewa nini.Laandika:

“Viwanda hivyo havidai hivyo bila sababu.Vinataka kuzima na mapema kuja baadae kuwekewa vikwazo vikali.

Mfumo ulioanzishwa Uingereza wa alama za rangi-nyekundu-kijani na manjano –unaeleweka na wateja bila kuhitaji kuwa wataalamu wakubwa wa hesabu.Bidhaa zenye dhara ya afya zinapewa alama nyekundu.Zile zenye afya zapewa alama ya kijani na zile zinazopakana na pande mbili za mwanzo zachukua rangi ya njano.

Kufanya hivyohivyo,Ujerumani kungezusha mstuko madukani kwenye supermarkets pale wapokeafedha wakiona bidhaa zaonesha tu rangi nyekundu.Watoto wadogo watakuwa na hisia mbaya na wazee wao hata zaidi.”