1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa Copenhagen - Matumaini na Hofu

7 Desemba 2009

Mkutano wa Umoja wa Mataifa juu ya mabadiliko ya hali ya hewa duniani umefunguliwa leo hii mjini Copenhagen.Wajumbe kutoka nchi 192 kwa majuma mawili watajadili mkataba mpya wa kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa.

https://p.dw.com/p/KrlJ
Yvo de Boer, Exekutivsekretaer der Klimarahmen-Konvention der Vereinten Nationen (UNFCC), spricht am Donnerstag, 29. Mai 2008, auf dem Internationalen Transport Forum in Leipzig. (AP Photo/Eckehard Schulz) ---- Yvo de Boer, Executive Secretary of the UNFCC, holds a keynote during the opening session of the International Transport Forum in Leipzig, eastern Germany, Thursday, May 29, 2008. (AP Photo/Eckehard Schulz)
Yvo de Boer, Mkuu wa masuala ya mazingira wa Umoja wa Mataifa.Picha: AP

Suala kuu ni, kwa kiwango gani nchi zilizoendelea kiviwanda zinapaswa kuzisaidia nchi zinazoendelea kujirekebisha kuambatana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Jambo moja limeshadhihirika: huu utakuwa mkutano mkubwa kabisa wa kimataifa kushuhudiwa ulimwenguni. Mpaka sasa wajumbe 15,000 wameitikia mwaliko wa kuhudhuria mkutano huo katika mji mkuu wa Danemark Copenhagen. Zaidi ya marais na viongozi wa serikali 100 watahudhuria mkutano huo katika siku za mwisho za majadiliano - Hii ni mara ya kwanza kabisa kwa viongozi wengi kama hao kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa juu ya mabadiliko ya hali ya hewa. Mkutano huo wa viongozi 100 unatazamiwa kuukomboa ulimwengu.

Kwa bahati mbaya lakini, siku chache kabla ya kufunguliwa kwa mkutano wa Copenhagen, data za siri za mchunguzi wa Kingereza zimevuja hadharani zikiashiria kuwa baadhi ya matokeo ya uchunguzi yamerekebishwa ili kutoa picha ya kutisha kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa. Hiyo bila shaka iliwafurahisha wale walio na wasiwasi kuhusu madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa na wakikanusha kabisa kuwa binadamu ndio wa kulaumiwa kuhusu ongezeko la joto duniani. Lakini watu wenye fikra kama hizo ni wachache kwani mtindo uliopo hivi sasa unaelekea dira moja tu - tunapaswa kuchukua hatua, si kwa ajili yetu, bali kwa vizazi vitakavyofuata.

Na hilo ndio linalokwamisha majadiliano ya sasa- kufikiria kile kitakachotokea baadae. Mabishano huzuka kuhusu fedha na sheria zinazoathiri bajeti zetu leo hii au suala la kupunguza uzalishaji wa gesi zinazochafua mazingira au kuwa waangalifu katika kutumia maliasili duniani. Tutachelewa sana ikiwa tutangojea mpaka mti wa mwisho utakapofyekwa na tone la mwisho la mafuta kuchimbuliwa ardhini - ikiwa tutafikiria tu yale yatakayotuathiri sisi wenyewe na sio wajukuu wetu.

Binadamu, katika kujipatia ustawi wa maisha, hasa katika nchi zilizoendelea kiviwanda, wameifanya anga kuwa jaa. Lakini wanaoathirika zaidi ni wale wasiohusika na uchafuzi huo wa mazingira. Kwa hivyo, lazima kuwepo haki katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.Nchi zilizoendelea kiviwanda na zilizosababisha madhara, zinapaswa kuwajibika. Na hiyo inawezekana haraka kwa kutumia fedha na teknolojia. Nchi zinazojaribu hivi sasa kuleta ustawi kwa umma wake, zisifanye makosa yale yale. Na nchi zilizoendelea kiviwanda, zinapaswa kuzisaidia nchi zinazoendelea.

Kwa hivyo katika mkutano wa Copenhagen ni lazima kupatikane makubaliano yatakayo ahidi haki ya kutumia kiwango maalum cha kaboni dayoksaidi, ikiwa ni Muhindi,Mrusi,Mjerumani au Mnigeria. Vita dhidi ya umasikini na ulinzi wa mazingira, ni matatizo makuu kabisa yanayohitaji kupatiwa ufumbuzi katika karne ya hivi sasa.Na safari hii mjini Copenhagen, yapo matumaini ya kupatikana makubaliano na kuziwajibisha nchi zilizohudhuria kuheshimu mkataba huo.

Mwandishi: H.Böhmke/ZPR

Mhariri: M.Abdul-Rahman