1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bonn Klimakonferenz

Sekione Kitojo9 Aprili 2010

Mkutano wa siku tatu wa hali ya hewa mjini Bonn umeanza kwa vikundi mbali mbali vinavyowakilishwa kushutumiana.

https://p.dw.com/p/Ms82
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon alipokuwa akijibu maswali ya waandishi habari katika mkutano uliopita wa hali ya hewa huko Copenhagen Denmark.Picha: AP

Mataifa wanachama wa umoja wa mataifa yatakuwa mjini Bonn hadi siku ya Jumapili yakihudhuria mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa, katika kutayarisha utaratibu kwa ajili ya mkutano mwingine wa hali ya hewa utakaofanyika mwezi Desemba nchini Mexico.

Matumaini ya kufanyika mkutano utakaoleta hatua za kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa kutokana na mkutano ulioshindwa mwezi Desemba mjini Copenhagen umepata pigo la mapema katika mazungumzo ya mjini Bonn yaliyoanza leo Ijumaa.

Katika mkutano wa kwanza tangu ule uliozusha jazba mwezi Desemba mjini Copenhagen , hakuna muafaka uliojitokeza miongoni mwa vikundi 194 vilivyomo katika utaratibu wa jukwaa la umoja wa mataifa linalohusika na kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa ( UNFCCC) ili kutayarisha njia na hali imechafuliwa tena na kunyoosheana vidole.

Kitu kimoja ambacho tunajifunza kutokana na historia ni kwamba hatujifunzi kutoka historia, amesema Tosi Mpanu Mpanu kutoka jamhuri ya kidemokrasi ya Congo akiwakilisha mataifa ya Afrika. Mkutano wa Copehagen umeharibu hali ya kuaminiana ambayo ni muhimu kwa uhusiano wa aina yoyote.

Jan Kowalzig kutoka katika shirika la Oxfam nchini Ujerumani ambaye amekuwa akihudhuria vikao vya kamati hiyo ya umoja wa mataifa kwa muda mrefu, amesema kuwa ni muhimu kwanza kuwa na mpango maalum kwa ajili ya mwaka 2010 ambapo kwa ajili hiyo wanachama wa kundi hili la mataifa 194 ya umoja wa mataifa wanakutana hapa mjini Bonn.

Ndipo linakuja swali, tunahitaji kujadili nini katika mwaka huu, na majadiliano hayo yafanyike wapi, wakati utakapofanyika mkutano wa hali ya hewa mwishoni mwa mwaka huu huko Cancun nchini Mexico.

Mkutano huu wa siku tatu katika mji mkuu wa zamani wa Ujerumani magharibi unafanyika karibu miezi minne baada ya mkutano ambao , baada ya kupigiwa upatu kuwa ni wakati ambapo binadamu watakusanya nguvu zao kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa , ulifikia karibu na kuwa maafa.

Wajumbe wanaohudhuria mkutano wa Bonn , walikuwa na miezi karibu mitatu ya kuweza kuuweka sawa mkutano ulioharibika wa Copenhagen. Wakati huo huo hata mkuu wa sekretariati ya umoja wa mataifa kuhusiana na mkutano huo wa hali ya hewa Yvo de Boer, amesema kukamilisha ripoti yake kuhusu mkutano wa Copenhagen na pia mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo hukosoa sana kama Oxfam, WWF na German Watch yamekubali, kuwa licha ya kutopatikana mkataba mwezi Desemba , kuna maeneo ambayo washirika waliokuwapo katika mkutano wa Copenhagen wanakubaliana.

Kuna maeneo ya majadiliano , ambapo hali inaridhisha, ambapo mtu anaweza kuwa na hisia, kuwa kila mtu anaona inawezekana. Kwa mfano katika kupitisha matokeo ya mabadiliko ya hali ya hewa katika mataifa yanayoendelea, ulinzi wa misitu ya mvua, matatizo ya utoaji gesi zinazoharibu mazingira ambazo zinaharibu misitu ya mvua, pia kama suala la kuhamisha tekonolojia pamoja na uwezeshaji.

Mambo mengine ambayo yanajadiliwa katika mkutano huu wa Bonn ni pamoja na ni mikutano mingapi mingine ya ziada itakayofanyika kabla ya mkutano wa Cancun na iwapo hatua zinapaswa kuchukuliwa kutayarisha muswada wa majadiliano katika muda wa wiki zijazo.

Mwandishi Jeppesen , Helle / ZR/ Kitojo Sekione

Mhariri:

ENDE