1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa hali ya hewa Copenhagen wamalizika

Sekione Kitojo20 Desemba 2009

Baada ya siku 13 za jitihada za kupata makataba wa makubaliano ya kupunguza uchafuzi wa mazingira, mkutano wa umoja wa mataifa wa hali ya hewa umemalizika mjini Copenhagen.

https://p.dw.com/p/L980
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa akizungumza jambo katika mkutano na waandishi habari katika mkutano wa mazingira mjini Copenhagen.Picha: AP

COPENHAGEN

Baada ya siku 13 za jitihada za kupata mkataba wa makubaliano, mkutano wa Umoja wa Mataifa wa hali ya hewa umemalizika mjini Copenhagen. Wajumbe wanakiri kwamba makubaliano yaliyoafikiwa jana, hayakutimiza malengo yaliyokuwa yamewekwa. Licha ya kuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon aliueleza mkataba huo wa Copenhagen kuwa ni hatua muhimu ya kwanza , lakini akasema bado kuna kazi kubwa.

Pamoja na hayo makubaliano hayo ya Copenhagen kwa mara ya kwanza , yanaweka malengo ya kupunguza ujoto kwa nyuzi joto mbili na kuahidi kitita cha dola bilioni 100 kuyasaidia mataifa maskini kupambana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa. Mkutano huo ulioyaleta pamoja mataifa 193 katika mji mkuu wa Denmark Copenhagen ulimalizika kwa kufikiwa mkataba ambao hauwajibishi kisheria uliokubaliwa na viongozi wa Marekani, China India, Brazil na Afrika Kusini. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel alielezea kutoridhishwa kwake na udhaifu wa mkataba huo, akisema uamuzi huo ulikuwa mgumu sana kwake binafsi.