1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa kilele kuhusu hali ya hewa

Oumilkher Hamidou29 Machi 2009

Rais Barack Obama apania kupigania usafi wa mazingira

https://p.dw.com/p/HM9j


Washington:

Rais Barack Obama wa Marekani amewaalika viongozi wa mataifa 16 yenye nguvu zaidi za kiuchumi ulimwenguni wahudhurie mkutano wa kilele kuhusu hali ya hewa utakaofanyika mjini Washington.Msemaji wa ofisi ya rais wa Marekani amesema kongamano kuhusu "Nishati na Hali ya hewa" litakalofanyika April 27 hadi 28 ijayo limelengwa kurahisisha njia ya kufikiwa makubaliano ya Umoja wa Mataifa ya kupambana na kuzidi hali jumla ya ujoto ulimwenguni.Mikakati madhubuti inategemewa kwa lengo la kuzidisha juhudi za kubuni nishati safi na kupunguza moshi wa sumu unaotoka viwandani.Kongamano hilo litakua kama maandalizi ya mkutano muhimu wa kilele utakaoitishwa July mwaka huu nchini Italy.Mbali na Marekani na Ujerumani,mataifa mengine pia ya Umoja wa Ulaya na Umoja wa mataifa yanatazamiwa kuhudhuria.Miongoni mwa walioalikwa ni pamoja na viongozi wa kutoka Australia,Brazil,Uengereza,Canada,China,Ufaransa,India,Indonesia,Italy,Japan,Korea,Mexico,Urusi,Afrika Kusini na Danemark.