1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya

Susanne Henn - (P.Martin)15 Oktoba 2008

Viongozi wa nchi na wa serikali za wanachama 27 wa Umoja wa Ulaya wamekusanyika kwa mkutano wa kawaida wa siku mbili mjini Brussels Ubeligiji.

https://p.dw.com/p/FZmo
European Commission President Jose Manuel Barroso arrives for an EU summit in Brussels, Monday Sept. 1, 2008. EU leaders will assess the impact of their fraying relations with Moscow at a summit on Monday, however they face limited options to punish Russia for invading Georgia and recognizing the independence of its Abkhazia and South Ossetia provinces. (AP Photo/Michel Euler)
Rais wa Komisheni ya Umoja wa Ulaya,José Manuel Barroso.Picha: AP

Mbali na mgogoro wa fedha,mkutano huo utashughulikia pia masuala ya ulinzi wa hali ya hewa,hatima ya mkataba wa Lisbon na uhusiano kati ya umoja huo na Urusi.Ingawa mgogoro wa fedha bado haujamalizika,viongozi wa nchi na wa serikali za nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya walipumua kidogo walipoelekea Brussels.Kwani ule mpango uliokubaliwa na nchi zinazotumia sarafu ya Euro katika mkutano maalum ulioitishwa Paris Ufaransa Jumapili iliyopita,umesaidia kupandisha bei za hisa katika masoko ya fedha.

Sasa ndio viongozi wa nchi wanachama 27 wa Umoja wa Ulaya kwa pamoja wanataka kushughulikia hatua za kudumu zitakazosaidia kutuliza masoko ya fedha.Licha ya kuwa kila nchi itaendelea na mpango wa kitaifa juu ya njia za kupambana na mgogoro wa masoko ya fedha duniani,Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesisitiza umuhimu wa kushauriana.Amesema:

"Ni vyema kuwa miongoni mwetu barani Ulaya-kuanzia Ufaransa, Hispania hadi Uingereza- tunachukua hatua za pamoja. Tunachohitaji kutambua ni kuwa njia pekee iliyopo ni kushirikiana."

Inatazamiwa kuwa hata nchi 12 zingine katika Umoja wa Ulaya zitafuata mwongozo ulioidhinishwa na zile zinazotumia sarafu ya Euro pamoja na Uingereza.Hadi hivi sasa katika Umoja wa Ulaya serikali za nchi 13 zimetoa fedha na dhamana kwa mikopo iliyopindukia Euro trilioni mbili.Hata ikiwa mgogoro wa masoko ya fedha unapewa kipaumbele katika majadiliano ya mjini Brussels,mkakati wa Umoja wa Ulaya kuhusu njia za kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani usipunguziwe umuhimu.Hayo alisisitiza Rais wa Komisheni ya Umoja wa Ulaya Jose Manuel Barroso.Akaongezea:

"Tatizo la mabadiliko ya hali ya hewa halitotoweka kwa sababu ya mgogoro wa fedha uliopo.Kwa hivyo lazima tutimize malengo yaliyokubaliwa kwa pamoja."

Lakini makubaliano kamili kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa na hata nishati,yanatazamiwa kukamilishwa kwenye mkutano wa Baraza la Ulaya utakaofanywa mwezi wa Desemba.Nchi nyingi kama vile Italia,Poland na Ujerumani zingependelea kuwa na sheria zisizo kali sana.Hata hatima ya mkataba mpya wa mageuzi wa Umoja wa Ulaya,utapewa umuhimu kwenye mkutano wa viongozi Desemba ijayo.