1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa kimataifa kuhusu UKIMWI kuanza leo Mexico City.

3 Agosti 2008
https://p.dw.com/p/Epm7

Mexico-City:

Mkutano mkubwa wa kimataifa katika historia ya miaka 27 ya janga la Ukimwi unafunguliwa leo katika mji mkuu wa Mexico.

Kabla ya kuanza mkutano huo, maelfu ya wanaharakati wameandamana kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, kulaani ubaguzi dhidi ya wahanga wa ugonjwa huo. Jumla ya washiriki 22.000-wanasayansi, waandaaji sera na watoaji huduma -wanakusanyika kwa mkutano huo wa siku sita utakaofunguliwa na katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon. Pia rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton anatarajiwa kushiriki. Watu wapatao 33 milioni duniani kote wamekumbwa na ugonjwa huo.

Katika bara la Afrika kusini mwa jangwa la Sahara Ukimwi ni chanzo cha vifo vya mamilioni wenye ukosefu wa dawa na matibabu ya kutosha.Duniani kote, watu milioni mbili hufariki dunia kila mwaka kwa sababu ya Ukimwi na nchioni Marekani maafisa wanasema takriban watu 56.000 wanaambukizwa ukimwi kila mwaka,ikiwa ni asili mia 40 zaidi kuliko makadirio ya hapo awali nchini humo.