1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa kimataifa wa ukimwi waanza Vienna

Josephat Nyiro Charo19 Julai 2010

Wanaharakati wa kupambana na ugonjwa wa ukimwi wametakiwa kuitumia kila senti kwa manufaa ya kupambana na virusi vya HIV, na sio kutaraji kuwa wafadhili watakuwa wanatoa tu hela na wala hazitumiwi ipaasavyo

https://p.dw.com/p/OPP6
Ukumbi wa mkutano wa ukimwi Vienna AustriaPicha: AP

Huu ndio ujumbe waliofika nao, rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton na Bill Gates katika mkutano wa kimataifa wa ukimwi mjini Vienna, Austria. Umoja wa Mataifa kwa upande wake umesema katika mwaka uliopita, kiasi ya watu milioni 1 na laki mbili walifanikiwa kupata dawa za kupunguza makali ya HIV.

Baadhi ya ajenda zilizokuwa katika mkutano huo wa kimataifa kuhusiana na ugonjwa ilikuwa ni pamoja na lile sisitizo la wanaoambukizwa virusi vya HIV kuanza kutumia dawa mapema za kupunguza makali ya virusi hivyo- Mkutano huo ambao unawaleta pamoja wataalam wa ukimwi, wanaharakati na maafisa wa huduma ya afya- pia uliarifiwa kuwa idadi ya watu wanaopokea dawa imeongezeka lakini bado kuna idadi kubwa ambao hawana njia ya kupata dawa hizo za kupunguza makali ya HIV.

Lakini ilikuwa ujumbe wa Rais wa Zamani wa Marekani Bill Clinton pamoja na muasisi wa Kampuni ya Micrososft Bill Gates kuwa fedha zinazotolewa katika vita dhidi ya ukimwi zinakuwa hazitumiwa ipaasavyo- hasa katika maeneo ambayo fedha hizo zinahitajika sana.

'' Uliwmengu kwa sasa unakabiliwa na matatizo mengi, kwa hivyo ni rahisi sana kulalamikia serikali kwa kutaka kupewa fedha zaidi, lakini lazima wanaharakati nao wabebe dhamana ya kutumia fedha hizo namna inavyohitajika, alisema Bill Clinton.

Aids-Kongress in Wien
Rais wa zamani wa Mareklani, Bill Clinton akiuhutubia mkutano wa Vienna Jumatatu Julai 19Picha: AP

Kiongozi huyo wa zamani wa Marekani aliwaambia wajumbe katika mkutano huo wa Vienna, iwapo mataifa ya wafadhili wataona matunda ya ufadhili wao- basi ni rahisi kunyoosha mkono na kuomba fedha zaidi kusimamia na kuendesa miradi mingi ya kupamaba na ugonjwa wa ukimwi.

Bill Gates ambaye wakfu wake wa hutumia hutumia kiasi kikubwa cha hazina yake ya kiasi ya dola bilioni 34 kupambana na ugonjwa wa ukimwi alisema uwajibikaji ndio msingi wa kuwezesha idadi ya watu milioni 15 wanaohitaji dawa za kupunguza makali ya virusi vya HIV kupata dawa hiyzo.

Shirika la afya duniani WHO nalo kwa upande wake limesema idadi ya watu wanaopokea matibabu imeongezeka kama robo, mwaka uliopita. Wakitoa takwimu mkutanoni humo WHO ilisema hadi mwishoni mwa wmwaka jana watu milioni 5 na laki mbili wanapata matibabu ya virusi vya HIV- idadi hii iliongezeka kwa milioni 1.2 katika kuanza kwa mwaka 2009.

Shirika hilo la afya ulimwenguni lilitoa wito kwamba juhudi zaidi zinahizajika kuwasishi wanaoishi na virusi vya HIV kutafuta matibabu mapema kabla ya kuathirika zaidi kiafya.

Wajumbe katika mkutano huo pia waliarifiwa kuwa hadi sasa watu kiasi ya milioni 33 wanaishi na virusi vya HIV na Ukimwi kote duniani. Umoja wa Mataifa nao unasema watu milioni 15 wanahitaji dawa za kupunguza makali ya HIV.

Mwandishi: Munira Muhammad/ afpe

Mhariri: Josephat Charo.