1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa mabadiliko ya tabia-nchi wamalizika Bonn

17 Juni 2011

Mkutano wa Kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi umemalizika mjini Bonn, Ujerumani hii leo (17.06.2011), kwa kufikiwa maazimio ya mpango wa fidia za maafa ya mazingira kwa mataifa yanayoendelea kutoka mataifa tajiri.

https://p.dw.com/p/11e5l
Mkuu wa Sekreteriati ya Mazingira ya Umoja wa Mataifa, Christiana Figueres
Mkuu wa Sekreteriati ya Mazingira ya Umoja wa Mataifa, Christiana FigueresPicha: DW

Mkutano huu uliandaliwa na Umoja wa Matafa ulidhamiria kutafuta muafaka wa namna ambavyo mataifa yaliyoendelea na yanayoendelea yanavyoweza kushirikiana kuutimiza Mkataba wa Ulinzi wa Mazingira wa Kyoto, hasa katika suala zima la uzalishaji wa gesi-joto zinazohatarisha tabaka hewa na hivyo kuathiri mabadiliko ya tabia-nchi.

Mohammed Khelef amezungumza na mmoja wa washiriki wa mkutano huo, Bwana Richard Muyungi, ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira, anayeshughulikia Mabadiliko ya Tabianchi, katika Ofisi ya Makamo wa Rais wa Tanzania, kuhusiana na mambo yaliyokubaliwa kwenye mkutano huo.

Mahojiano: Mohammed Khelef/Richard Muyungi
Mhariri: Othman Miraji