1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa mabalozi wa Ujerumani

10 Septemba 2008

Mkutano wa mabalozi wa Ujerumani mjini Berlin.

https://p.dw.com/p/FFNV
Walter SteinmeierPicha: picture-alliance/dpa

Mara moja kwa mwaka mabalozi wa Ujerumani wanaotumika nchi za nje hukutana katika wizara ya nje mjini Berlin.Huondoka katika afisi zao za Ubalozi ama mjini Beijing,Mexico City au Lisbon ili kubadilishana maarifa na mawazo kwa muda wa siku 4 kwenye mkutano wao wa mabalozi.Siku moja kati ya hizo 4 wanajishughulisha na maswali ya kiuchumi.Kikao cha mwaka huu kimetuwama juu ya bara la Afrika.

Kiasi cha waakilishi 1000 wa viwanda na wa fani mbali mbali za uchumi wamealikwa kwenda Berlin kuhudhuria kikao hiki na waziri wa nje wa Ujerumani Bw.Frank-Walter Steinmeier.

"Ni jukumu la siasa ya nje na ajenda ya waziri wa nje kufungua milango, upeo pamoja na njia za jinsi ya kuingilia masoko ya nje na kusaidia kusaka washirika wa kushirikiana nao.Pia ni jukumu lake kupigia debe bidhaa "Made in Germany"- bidhaa zilizotengezwa Ujerumani."

Katika mkutano huu wa mabalozi wa Ujerumani hukutana wanasiasa wa Ujerumani wanaotumika nchi za nźgambo,mabalozi ,makonsul na wanabiashara na wanaviwanda.

Kikao cha mwaka huu macho yamekodolewa bara la Afrika.

Romy Rosnedr ni muakilishi wa Jumuiya ya Afrika na Ujerumani ya wanaviwanda anasema:

"Upepo mpya unavuma hivi sasa.Kuna nchi nyingi zilizo imara sana tangu kisiasa hata kiuchumi na zinatoa uwezekano mkubwa wa kutia raslimali."

Fursa hizo ziliopo pia lakini zina shida zake: Mara nyingi inatokea tatizo la rushua linalokabili makampuni au viwanda vinavyotaka kuekeza.Pia kuna kasoro za usalama wa kisheria kutoa kinga kampuni linapotaka kununua ardhi au nyumba.

Mkakampuni yanatarajia msaadw a wajumbe wa kibalozi hasa kurahisishiwa viza za kusafiria tena tangu kwa wajerumani wanaotaka kusafiri nje lakini pia kwa washirika wao wa kibiashara wanaotoka ngambo wakitaka kuja Ujerumani.

Wolfgang Gohde kutoka kampuni la PARTEC aliwaomba mabalozi msaada wao katika kuwasiliana na wizara lakini pia katika kugombea kandarasi zinazochapishwa hadharani.

Bw.Gohde qanauza sehemu mbali mbali za dunia zana za ufundi wa hali ya juu za matibabu,Zana za kutambua maradhi kama vile ya UKIMWI,malaria na kifua kikuu.Soko lake muhimu sana ni Afrika:

Anasema,

"Ujerumani ina jina zuri barani Afrika na kuna nyakati unapata hisia wanasiasa hawalitumii jina hilo kubwa ilionalo ipasavyo.Wafaransa,wabelgiji na waingereza lakini,wanatumia kwa werevu zaidi."

Wanaviwanda wa Ujerumani wamejitembeza mbele ya mabalozi hao wa Ujerumani kifua mbele.Wametamba kuwa wao ,ndio mabingwa wa dunia wanaoongoza kuuza bidhaa nyingi nchi za nje.Mwaka uliopita wameuza nje bidhaa za thamani ya Euro bilioni 1000.

Kwa makampuni na viwanda vingi vya Ujerumani anasema makamo-rais wa shirikisho lao Arend Oetker,biashara na nchi za nje inazidi kuongeza umuhimu wake.Kwani mara nyingi inatokea zaidi ya nusu ya biashara ya Ujerumani inafanywa na nchi za nje.