1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa mazingira waanza.

3 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CWJj

Bali. Mkutano mkubwa uliotayarishwa na umoja wa mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa unaendelea katika kisiwa cha Bali nchini Indonesia. Mkutano huo utakaofanyika kwa muda wa siku 11 unahudhuriwa na zaidi ya mataifa 180. Mkutano huo una lengo la kuanzisha rasmi mazungumzo juu ya mkataba wa hali ya hewa unakaokuwa badala ya ule wa Kyoto, ambao unamaliza muda wake mwaka 1012. Wakati wa ufunguzi wa mkutano huo mwenyekiti wa mkutano Yvo de Bear amesema mada hiyo ni magumu lakini inajadilika.

Mazungumzo hayo ya Bali yamepata msukumo wakati waziri mkuu mpya wa Australia Kevin Rudd alipoidhinisha makubaliano hayo ya Kyoto ikiwa ni hatua yake ya kwanza kuichukua baada ya kuapishwa kuwa kiongozi wa nchi hiyo kufuatia uchaguzi uliofanyika mwezi uliopita. Hatua hiyo ya Rudd inaiacha Marekani kuwa nchi pekee ya viwanda ambayo bado haijaidhinisha makubaliano hayo. Ujumbe wa Marekani umesema kuwa hautakuwa kikwazo kwa makubaliano mapya ya hali ya hewa, lakini Marekani inaendelea kupinga hatua ambazo nchi nyingi zinaunga mkono , kama vile upunguzaji wa lazima wa utoaji gesi zinazochafua mazingira na malengo ya kuweka viwango maalum katika ongezeko la ujoto duniani.