1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa Tabia nchi mjini Cancun Mexico.

30 Novemba 2010

Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Tabia nchi umeanza mjini Cancun, Mexico.

https://p.dw.com/p/QLTJ
Nembo ya mkutano wa Cancun

Awamu mpya ya mazungumzo ya tabia nchi ya Umoja wa Mataifa imeanza nchini Mexico. Ni takriban mataifa 200 yanayokutana mjini Cancun yakiwa na matumaini ya kufikia makubaliano kuhusu masuala muhimu yanayozigawana nchi tajiri na zile zinazoinuka kiuchumi.

Kamishna wa tabia nchi wa Umoja wa Ulaya,Conie Hedegaard amesema itakuwa muhimu kwa nchi tajiri duniani kufanya maendeleo la sivyo baadhi ya washirika watakosa kuuvumilia mpango wa Umoja wa Mataifa.

Vor UN-Klimagipfel in Cancun - Connie Hedegaard
Kamishna wa Tabia nchi wa Ulaya Connie Hedegaard.Picha: picture-alliance/dpa

Umoja wa Ulaya utakuwa ukishinikiza makubaliano  ya jinsi ya kuzisaidia nchi maskini kuyazoea mabadiliko ya tabia nchi na jinsi ya kubadilishana teknologia zinazohusika na tabia nchi.

Hatahivyo Hedegaard ameonya kwamba Umoja wa Ulaya utakataa  kuongeza muda wa makubaliano ya Kyoto iwapo nchi nyingine hazitotia saini kukubali kupunguza viwango vya utoaji wa gesi.

Mwandishi :Maryam Abdalla/Ape,Dpae,Rtre.