1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa Umoja wa Mataifa juu ya hali ya hewa.

Abdu Said Mtullya23 Septemba 2009

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon asema mafanikio katika kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa yataleta neema duniani.

https://p.dw.com/p/Jmnx
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon.Picha: AP

NEW YORK:

Rais wa China Hu Jintao amesema nchi yake itapunguza kwa kiwango kikubwa, gesi zinazoharibu mazingira hadi kufikia mwaka 2020.

Rais Hu Jintao alitoa ahadi hiyo kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa juu ya hali ya hewa unaohudhuriwa na viongozi wa nchi na serikali kutoka duniani kote. Hatahivyo, ameambatanisha ustawi wa uchumi wa nchi yake na utekelezaji wa ahadi hiyo.

Hapo awali katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki-Moon alisisitiza ulazima wa kutoa ishara ya nia njema kama msingi wa kuleta mafanikio kwenye mkutano wa mjini Copenhagen utakaofanyika mwezi desemba.

Wajumbe kwenye mkutano huo watajadili mkataba mpya wa kimataifa juu ya ulinzi wa hali ya hewa utakaochukua nafasi ya rasimu ya Kyoto.

Katibu mkuu Ban Ki -Moon amesema kupitishwa mkataba huo mpya kutakuwa na maana ya kuleta neema ,usalama na haki zaidi.