1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa usalama mjini Munich

9 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D4tZ

München:

Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyib Erdogan amefungua mkutano wa 44 wa kimataifa kuhusu usalama katika mji mkuu wa jimbo la kusini la Ujerumani Bavaria.Ameshadidia umuhimu wa nchi yake katika siasa za ulimwengu,.Amesema hali iliyosababishwa na mashambulio ya september 11 mwaka 2001 inaishughulisha pia nchi yake.Wawakilishi 250 wa ngazi ya juu kutoka mataifa 50,akiwemo waziri wa ulinzi wa Marekani Robert Gates na makamo wa rais wa Urusi Sergei Ivanov wanahudhuria mkutano huo.Ujerumani inawakilishwa na waziri wa ulinzi Franz Josef Jung na waziri wa mambo ya nchi za nje Frank-Walter Steinemeier.Mada kuu mkutanoni ni kuhusu Afghanistan,kudhibitiwa mbio za kujirundikia silaha na uhusiano kati ya nchi za magharibi na Urusi.Suala la Afghanistan liligubika pia mkutano wa siku mbili wa mawaziri wa ulinzi wa jumuiya ya kujihami ya magharibi NATO uliomalizika jana mjini Vilnius nchini Lithuania.