1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa Usalama wa Kimataifa

P.Martin8 Februari 2008

Mkutano wa Usalama wa Kimataifa wa 44 unafunguliwa leo jioni mjini Munich,kusini mwa Ujerumani chini ya kauli-mbiu "Ulimwengu ulio katika Vurugu".

https://p.dw.com/p/D4L1
***VB NATO Verteidungsmin. -Beratungen zur Lastenverteilung bei der Militäroperation in Afghanistan, Riegert*** Bundesverteidigungsminister Franz Josef Jung (CDU) äußert sich am Mittwoch (06.02.2008) auf einer Pressekonferenz in Berlin zum Afghanistaneinsatz der Bundeswehr. Der US-amerikanische Verteidigungsminister hatte gefordert, dass sich die deutschen Streitkräfte auch an Kampfhandlungen im Süden des Landes beteiligen sollten. Foto: Tim Brakemeier dpa/lbn +++(c) dpa - Report+++
Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani,Franz-Josef Jung akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari kuhusu ujumbe wa AfghanistanPicha: picture-alliance/ dpa

Ujumbe wa kijeshi wa madola shirika nchini Afghanistan,ni mada itakayotawala mkutano huo.Kama wajumbe 350 watahudhuria dhifa itakayofungua Mkutano wa Usalama wa Kimataifa leo jioni mjini Munich. Mkutano huo unawaleta pamoja maraisa,mawaziri wakuu na zaidi ya mawaziri 40 wa masuala ya nje na ulinzi.

Lakini mkutano huo umegubikwa na mvutano wa NATO unaohusika na ujumbe wake wa kijeshi katika Afghanistan. Bila shaka Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Franz-Josef Jung atajikuta akitetea tena msimamo wa Ujerumani kuhusu Afghanistan.

Washirika wa NATO: Uingereza,Marekani,Kanada na Uholanzi wakiwa na wanajeshi wao katika eneo la machafuko kusini mwa Afghanistan wanaishinikiza Ujerumani vile vile ipeleke vikosi vyake katika eneo hilo la mapambano.Lakini Jung anasema,majeshi yake yana mamlaka dhahiri kutoka Bunge la Ujerumani na kuna masikilizano pamoja na NATO kuwa dhamana yao hasa ni eneo la kaskazini la Afghanistan wanakosaidia miradi ya ukarabati na siko kusini mwa nchi hiyo.Akaongezea kwamba ni dhahiri kuwa mshirika akiwa na shida wapo tayari kusadia,kwani huo ni mshikamano uliopo katika NATO.

Bila shaka hayo ni maneno matamu kwa Katibu Mkuu wa NATO Jaap de Hoop Scheffer.Lakini kilicho muhimu zaidi kwake ni kuimarishwa idadi ya wanajeshi wa NATO kusini mwa Afghanistan.Suala linaloulizwa ni kwa muda gani zaidi Ujerumani na nchi zingine za Ulaya zitaweza kungángania kubakia kule zilipo.Kwani kwa maoni ya mwandalizi wa mkutano wa Usalama wa Kimataifa bwana Horst Teltschik, ujumbe wa NATO huko Afghanistan upo hatarini.Hata hivyo anasema NATO imenusurika na mizozo mingi na itaweza pia kuvumilia pigo nchini Afghanistan.

Lakini mkutano wa Munich hautoshughulikia Afghanistan tu.Jimbo la Serbia la Kosovo linalotaka kujitangazia uhuru wake hivi karibuni vile vile ni suala litakaloshughulikiwa.Kwani mkutano huo unatoa nafasi nzuri kwa Rais Boris Tadic aliechaguliwa nchini Serbia hivi karibuni,kuwa na mazungumzo yasio rasmi pamoja na viongozi wenzake pembezoni mwa mkutano .

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel aliewahi kushiriki katika mikutano miwili iliyopita,safari hii hatokuwepo.Lakini Naibu Kansela Frank-Walter Steinmeier alie pia Waziri wa Nje wa Ujerumani,bila shaka ataitumia fursa ya mkutano huo kupigia debe juhudi za kupunguza usambazaji wa silaha duniani.