1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa Viongozi wa Umoja wa Ulaya: Brussels

11 Desemba 2009

Mpango wa fedha kwa nchi zinazoendelea kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, kuendelea kujadiliwa.

https://p.dw.com/p/KzdN
Waziri mkuu wa Sweden, Fredrik Reinfeldt.Picha: picture-alliance/dpa

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanaoukatana mjini Brussels, wameshindwa kukubaliana na mpango wa kuyapa mataifa yanayoendelea Euro bilioni sita, kukabiliana na athari za ongezeko la ujoto duniani. Katika siku ya kwanza ya mkutano huo wa siku mbili, Waziri mkuu wa Sweden Fredrik Reinfeldt, ambaye nchi yake inashikilia urais wa Umoja huo, alisema viongozi hao wataendelea kujadiliana ili kukamilisha mpango huo.

Uingereza na Sweden zinaongoza kwa kutoa kiasi kikubwa cha fedha kufadhili mpango huo. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel alisema Ujerumani itachangia katika hazina hiyo, lakini hakusema kiasi nchi yake itakachotoa. Kuhusiana na malengo ya Umoja wa Ulaya, ya kupunguza viwango vyake vya gesi inayoharibu mazingira, kwa asilia mia 30, Reinfeldt, alisema pendekezo la Umoja huo, litategemea malengo watakayoweka Marekani na China.