1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa viongozi wa Umoja wa Ulaya mjini Bruxelles

Hamidou, Oumilkher19 Juni 2008

KUra ya La ya ireland na bei ya mafuta vinatishia kugubika mkutano wa kilele wa Umoja wa ulaya

https://p.dw.com/p/EN0J
Mwenyekiti wa halmashauri kuu ya Umoja wa ulaya Jose Manuel BarrosoPicha: AP


Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamepania kuyanusuru makubaliano ya Lisbone baada ya kura ya La" ya Ireland.Lakini kizungumkuti kinakutikana katika suala la namna ya kupunguza ughali uliokithiri wa bei ya mafuta ya petroli.


Viongozi wa taifa na serikali za nchi 27 za umoja wa ulaya,watakaoanza mazungumzo yao baadae leo usiku mjini Bruxelles,wanakutana katika wakati ambapo bunge la Uengereza limeshaidhinisha makubaliano ya Lisbone siku moja kabla.


"Uamuzi wa bunge la Uengereza wa kuidhinisha makubaliano ya Lisbone,ni wa 19 ndani ya Umoja wa ulaya" amesema spika wa bunge la ulaya Hans Gert Pöttering,akisifu kile alichokiita "ishara muhimu" itakayozitanabahisha nchi nyengine nane zilizosalia zifuate njia hiyo hiyo.


Na hilo ndilo viongozi wa Ulaya,akiwemo pia wa Ireland,wanalodhamiria kulifanya wakati wa mkutano wao wa siku mbili,hata kama hali isiyo bayana nchini Poland na katika jamhuri ya Tcheki inatishia kuparaganya mambo.


Lengo ni kupatikana nchi 26 zinazounga mkono makubaliano ya Lisbone yanayozungumzia haja ya kubuniwa wadhifa wa rais wa baraza la ulaya,kuteuliwa "waziri "wa mambo ya nchi za nje wa Umoja wa ulaya na kuwepo mfumo wa kura za walio wengi,kabla ya kuamuliwa nini cha kufanya.


"Itakua shida sana kuleta mageuzi ya taasisi," amesema hayo mwenyekiti wa halmashauri kuuya Umoja wa ulaya José Manuel Barroso.


Waziri mkuu wa Ireland Brian Cowen anaebidi kuwaeleza viongozi wenzake kwanini nchi yake imeyakataa makubaliano ya Lisbone,hakubisha,ingawa amekwepa kutoa pendekezo lolote la kuikwamua hali iliyoko.


"Ni mapema mno kuweza kusema ufumbuzi wa aina gani ndio wa maana,sio tuu kwa Ireland bali kwa ulaya nzima" amesema hayo mwenmyekiti wa halmashauri kuu ya umoja wa ulaya Jose Manuel Barroso wakati wa mkutano pamoja na wanadishi habari hii leo mjini Bruxelles.


Washirika wa umoja wa ulaya wanakubaliana Ireland inabidi ipatiwe muda.


 Kuna wanaozungumzia kipindi cha hadi October ,japo kama mambo mawili muhimu yanasubiriwa October 15 na 16, ambapo makubaliano ya Lisbone yatakua yameshaidhinishwa au muda wa  kuidhinishwa utakua unakurubia kumalizika.


La pili ni uchaguzi wa bunge la Ulaya June mwakani.Viongozi wote wa Umoja wa ulaya wanakubaliana ufumbuzi lazma uwe umeshapatikana kabla ya tarehe hiyo.


Mada nyengine tete mazungumzoni inahusu malumbano kati ya Ujerumani na Ufaransa kuhusu mafuta ya petroli.Wadadisi wanahisi ikiwa viongozi wa umoja wa ulaya wanakubaliana juu ya haja ya kuyanusuru makubaliano ya Lisbon,kishindo ni kikubwa zaidi linapohusika asuala la namna ya kukabailiana na kuzidi kupanda bei ya mafuta ya petroli.


Ufaransa itakayoshika zamu ya mwenyekiti wa umoja wa ulaya kuanzia July mosi ijayo inataka fedha zinazopatikana kutokana na kodi ziada za bidhaa zitumike kusawazisha bei ya mafuta kwa wakulima,na wavuvi.


Fikra hiyo inapingwa na wengi miongoni mwa viongozi wa Umoja wa ulaya.


Kwa mfano kansela Angela Merkel wa Ujerumani aliyeshauri bungeni mjini Berlin  hii leo"watu wajiepushe kutumia fedha za malipo ya kodi.