1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa wafadhilio wa Palastina kesho mjini Paris

Oummilkheir16 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CcLF

Paris

Wawakilishi wa jumuia ya kimataifa wanakutana kesho mjini Paris kuzungumzia namna ya kuunga mkono kifedha uwezekano wa kuundwa taifa la Palastina.Wajumbe toka mashirika na nchi 90 wanatazamiwa kuhudhuria mkutano huo wa wafadhili uliolenga kukusanya dala bilioni tano nukta sita kusaidia mpango wa kiuchumi wa utawala wa ndani wa Palastina kwa kipindi cha mwaka 2008-2010..Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-Moon,waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Condoleezza Rice na waziri wa mambo ya nchi za nje wa Urusi wanatazamiwa kushiriki katika mkutano huo unaohudhuriwa pia na rais Mahmud Abbas.Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa ataufungua mkutano huo wa wafadhalili utakaosimamiwa baadae na waziri wake wa mambo ya nchi za nje Bernard Kouchner.Sambamba na mkutano huo wa wafadhili,wawakilishi wa pande nne zinazosimamia utaratibu mpya wa amani ya mashariki ya kati,watakutana pia kesho mjini Paris.Mikutano yote hii miwili inafuatia mkutano wa kimataifa kuhusu utaratibu wa amani kati ya Israel na Palastina uliotishwa Annapolisi Marekani mwezi uliopita.