1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa wakuu wa nchi za maziwa makuu waanza Lusaka

Josephat Nyiro Charo15 Desemba 2010

Mkutano huo wa kilele unanuia kukomesha makundi yenye silaha kupata nafasi ya kudhibiti madini

https://p.dw.com/p/QaQG
Rais wa Zambia, Rupiah BandaPicha: AP

Rais Rupiah Banda wa Zambia leo ameufungua mkutano wa kilele wa wakuu wa nchi za eneo la maziwa makuu mjini Lusaka, wenye wenye lengo la kudhibiti biashara haramu ya madini pamoja na mafuta ambayo imekuwa ikichangia mizozo kwenye eneo hilo.

Msemaji wa umoja huo wa ICGLR Liberata Mulamula amesema mkutano huo unadhamiria kukomesha makundi yenye silaha kupata nafasi ya kudhibiti madini.

Umoja huo wa nchi za eneola maziwa mkuu unajumuisha nchi 11, zikiwemo pia Kenya,Uganda , Ethiopea na Sudan.Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo hususan katika eneo la mashariki ni mfano wa jinsi madini ya almasi yalivyo chanzo cha mzozo, wakati ambapo nishati ya mafuta imekuwa chanzo huko Angola.