1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wajadili Uharamia

18 Aprili 2011

Viongozi wa serikali na viwanda kutoka zaidi ya nchi 50 wanakutana Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu kutafuta njia za kupambana na tatizo kubwa la uharamia linaloathiri binadamu na uchumi.

https://p.dw.com/p/RIml
A Yemeni coast guard mans a weapon, as his boat patrols the Gulf of Aden off the coast of Yemen, Monday, Dec. 1, 2008. The U.N. Security Council has extended for another year its authorization for countries to enter Somalia's territorial waters, with advance notice, and use "all necessary means" to stop acts of piracy and armed robbery at sea. Diplomats said the 15-nation council's unanimous resolution Tuesday is needed to stop the piracy off Somalia that threatens humanitarian efforts and regional security, and seems to be growing ever more audacious and technologically sophisticated each week.. (AP Photo/Mohammed al-Qadhi)
Mlinzi wa pwani akipiga doria katika Ghuba ya Aden nje ya mwambao wa YemenPicha: AP

Huu ni mkutano wa kwanza wa daraja ya juu kupata kufanywa kati ya serikali na makampuni binafsi katika kanda ya Ghuba, kujadili njia za kukomesha vitisho vya uharamia vinavyozidi kuenea. Mkutano huo wa siku mbili, ulioitishwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Umoja wa Ufalme wa Kiarabu na DP World-shirika la kimataifa linaloongoza shughuli za bandari, utajadili jithada za serikali na pia makampuni binafsi ya wamiliki meli, kukabiliana na madhara ya vitendo vya uharamia kwa mateka, familia zao, jamii kwa jumla. Vile vile vipi vitendo hivyo vya uharamia vinavyohatarisha amani na usalama kote duniani. Lengo, ni kuanzisha mpango wa ushirikiano kati ya pande zote mbili ili kuendeleza jamii,usalama na njia za kupeana habari.

Majopo maalum yatashughulikia kiini cha tatizo hilo la uharamia, masuala yanayohusika na sheria za kimataifa na uwezo wa kuendeleza ushirikiano wa kiraia na kijeshi ili kuzuia mashambulio ya maharamia. Pembezoni mwa mkutano huo, Umoja wa Falme za Kiarabu na Umoja wa Mataifa zitakuwa na kikao maalum cha kuchanga fedha kwa ajili ya mfuko maalum UN Trust Fund ulioanzishwa na Umoja wa Mataifa Januari mwaka 2010 kusaidia shughuli za kupiga vita uharamia katika mwambao wa Somalia.

Hasara kubwa kwa maisha na uchumi

Mutmaßliche Piraten in Somalia festgenommen.jpg Union of Islamic Courts (UIC) soldiers from the anti-piracy unit escort Somali nationals accused of hijacking a vessel in the port of Mogadishu, Somalia, Sunday 12, November 2006. The UIC rescued sailors from the vessel MV Veesham 1 and arrested a number of Somali's accused of hijacking the ship earlier in the week. UIC Chairman Sheikh Sharif Sheikh Ahmed said that the punishment of the pirates will end all piracy ambitions by outlaws in the region. EPA/ABUKAR ALBADRI +++(c) dpa - Report+++
Wasomali walioshukiwa kuteka nyara meliPicha: picture-alliance/dpa

Kwa mujibu wa Kituo cha Kimataifa cha Usafiri wa Baharini, tangu Aprili 14 mwaka huu 2011, kumetokea vituko 107 vya uharamia dhidi ya meli za shehena katika Ghuba ya Aden, Bahari ya Urabuni na nje ya mwambao wa Afrika Mashariki. Meli 17 zimetekwa nyara. Inatathminiwa kuwa hivi sasa maharamia wamezuia takriban meli 26 pamoja na wafanyakazi wake 532 wanaoishi katika hali mbaya. Mbali na hasara ya maisha ya binadamu, vitendo vya uharamia vinasababisha pia hasara kubwa katika biashara ya kimataifa ikitathiminiwa kufikia hadi dola bilioni 12 kwa mwaka.

Mkutano huo unaofanyika Dubai unahudhuriwa na mawaziri wa mambo ya nje wa takriban nchi zote za Ghuba na zile nchi zinazoathirika moja kwa moja kutokana na vitendo vya uharamia, kama vile Somalia, Djibouti,Comoro na Tanzania. Hata Naibu-Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na mawaziri wa nje wa Indonesia, Nigeria na Pakistan wanahudhuria mkutano huo.

Mwandishi: Aryam Abraha/DW Amh/Prema Martin

Mhariri:Abdul-Rahman