1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkuu wa jeshi la polisi Kongo asimamishwa kazi kwa mauaji ya Chebeya

Josephat Nyiro Charo7 Juni 2010

Maafisa kadhaa wa polisi wametiwa mbaroni kwa kuhusika na mauaji ya mwanaharakati huyo wa kutetea haki za binadamu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

https://p.dw.com/p/Nk4s
Floribert Chebeya, mwanaharakati wa kutetea haki za binadamuPicha: picture-alliance/ dpa/dpaweb

Mashirika ya kutetea haki za binaadam katika Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo yamepongeza hatua ya rais Joseph Kabila ya kumsimamisha kazi inspekta mkuu wa polisi ya nchi hiyo ili kuruhusu uchunguzi wa kifo cha mwanaharakati wa kutetea haki za binadamu, Floribert Chebeya, aliyeuliwa wiki iliyopita mjini Kinshasa. Hata hivyo, mashirika hayo yameomba uchunguzi zaidi na wa haki ufanyike ili kutathmini sababu za mauaji ya Bwana Chebeya.

Mhariri, Othman Miraji