1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkuu wa Umoja wa Afrika Jean Ping akutana na Mugabe

Kalyango Siraj5 Mei 2008

Marekani yatoa shinikizo kwa UA kuingilia kati

https://p.dw.com/p/Du3u
Morgan Tsvangirai, kiongozi wa chama cha upinzani Zimbabwe cha MDC asema atatoa msimamo wake kuhusu duru ya pili wakati tume ya uchaguzi itakapotangaza tarehe ya duru hiyo.Picha: AP

Rais wa halmashauri kuu ya Umoja wa Afrika,Jean Ping amefanya mazungumzo na rais Robert Mugabe kuhusu mgogoro wa uchaguzi wa nchi hiyo.

Ziara yake inakuja wakati mgogoro huo ukiwa umewagawanya viongozi wa Afrika.

Jean Ping,aliechaguliwa juzi kuongoza halmshaurikuu ya Umoja wa Afrika aliwasili Harare jumapili.Ingawa ratiba yake haikufahamika baado lakini,habari kutoka Harare mji mkuu wa Zimbabwe zinasema alikuwa akutane na rais Robert Mugabe.Suala kuu bila shaka huenda likawa mgogoro wa uchaguzi ambao unatishia amani ya nchi hiyo.

Hii ni kwa sababu ziara yake hii imekuja wakati kukiwa na shinikizo kadhaa kutoka Marekani,ikitaka Umoja wa Afrika kujihusisha zaidi nchini Zimbabwe ili kuupatia ufumbuzi mgogoro huo.

Matokeo ya uchaguzi wa urais ya Machi 29 ambayo yalicheleweshwa yalicheleweshwa kutolewa bila ya sababu inayoeleweka,hatimae yalitolewa rasmi wiki iliopita.Yanaonyesha kuwa kuna duru ya pili kati ya majogoo wawili,rais Mugabe na mpinzani wake mkuu Morgan Tsvangirai.

Upinzani unapinga duru ya pili ukisema kuwa haina maana,kama alivyosema mwishoni mwa juma,makamu wa rais wa chama cha Movement for Democratic Movement,MDC,Thokozani Khupe kuwa hawaoni haja ya kwenda katika duru ya pili ya uchaguzi wakiwa walishinda duru ya pili.

Upande wa Mugabe unashangilia hatua hii ukisema kuwa mara hii kiongozi wao atapata ushindi wa bayana

Wachambuzi wa masuala ya kisasa wanasema kuwa mgogoro huo sio tu umewagawanya viongozi wa Zimbabwe lakini pia na viongozi wengi barani Afrika,hususan wa mataifa ya kusini mwa Afrika ambao kawaida wamekuwa wakisaidiana dhidi ya kile wanachochukulia kama uingiliaji kati wa mataifa ya magahribi.

Mgawanyiko katika jumuia ya maendeleo ya mataifa ya kusini mwa Afrika ya SADC,inayoyaleta pamoja mataifa ya kikanda 14, ni kati ya serikali ambazo zinaongozwa na viongozi waliopigana vita vya ukombozi wakipinga wakoloni dhidi ya marais wanaofuata ajenda inaegemea nchi za magharibi.

Mhadhiri wa siasa katika chuo kikuu cha Zambia,Neo Simutayi,anasema kuwa kuna fikira miongoni mwa wazee kuwa mataifa ya magharibi yana nia ya kuwarithisha viongozi kama Mugabe na vikaragosi vya magharibi.

Ameongeza kuwa kizungumkuti ni kuwa viongozi vijana wanaanza kwenda kinyume na mwoyo wa ushikamano.

Mchambuzi huyo anasema kuwa kizazi kipya cha viongozi kijana huwa kinataka kuwalaani wenzao hadharani ikiwa mambo yameenda kombo katika nchi jirani.

Marais kama vileLevy Mwanawasa wa Zambia,akiungwa mkono na cheo somo wake kutoka Botswan Ian Khana na Jakaya Kikwete wa Tanzania ndio viongozi pekee wa jumuia hiyo ya SADC wanaotaka uingilaji kati katika mgogoro wa Zimbabwe.

Kwa mda huohuo mataifa jirani yameitaka serikali ya Zimbabwe kuhakikisha usalama ikiwa kutakuwa na duru ya pili ya uchaguzi wowote ule.

Haijulikani ikiwa kiongozi wa chama cha upinzani cha MDC atakubali duru hiyo.Lakini msemaji wake ,George Sibotshiwe ameliambia shirika la habari la Associated Press kuwa Tsvangirai atatoa kauli yake kuhusu duru ya pili baada ya tume ya uchaguzi kutangaza siku ya upigaji kura. Na haijulikana ikiwa uamuzi huo utakuwa wa ndio au hapana.