1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mogadishu. Maafa ya kiutu yanakaribia Somalia.

21 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC8b

Kundi moja la haki za binadamu nchini Somalia limesema kuwa kiasi cha watu 113 wameuwawa katika mapigano ya hivi karibuni katika mji mkuu Mogadishu kati ya majeshi ya serikali , yanayoungwa mkono na majeshi ya Ethiopia, na wapiganaji wa Kiislamu.

Hii inakuja wakati shirika la kuwahudumia wakimbizi la umoja wa mataifa limeonya kutokea maafa ya kiutu kutokana na kuendelea kwa ghasia na kushindwa kufikisha misaada kwa wale wanaoihitaji.

Umoja wa mataifa unakadiria kuwa zaidi ya Wasomali 300,000 wamekimbia makaazi yao mjini Mogadishu, wengi wao wakiwa wanawake na watoto ambao wanateseka kutokana na kukosa maji safi na chakula.

Maafisa wa umoja wa mataifa wanahofia kuwa magonjwa ya kipindupindu na kuhara yanaweza kuongeza hali kuwa mbaya zaidi.

Mwezi Desemba , majeshi ya Ethiopia yaliwaondoa wapiganaji wa Kiislamu kutoka mjini Mogadishu lakini mapigano yamezuka tena kuanzia mwezi uliopita na kusababisha watu 1,000 kuuwawa katika muda wa siku nne.