1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU: Mabaharia 24 wa Kiasia waachiliwa huru

5 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C79w

Maharamia wa Kisomali wamewaachilia huru mabaharia 24 wa Kiasia waliotekwa nyara mwezi wa Mei nje ya pwani ya Somalia.Boti mbili za uvuvi, zilizotekwa nyara ni mali ya Korea ya Kusini na sasa zimekwenda Yemen.Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Korea ya Kusini,maharamia hao wa Kisomali walidai kulipwa Euro laki tano hadi laki saba na nusu,lakini haijulikani ikiwa pesa hizo zimelipwa.Nje ya mwambao wa Somalia ni eneo lililo maarufu kwa vitendo vya uharamia.