1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU: Majeshi ya serikali yateka ngome ya mwisho ya wanamgambo nchini Somalia.

13 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCb2

Majeshi ya serikali ya Somalia, yanayosaidiwa na Ethiopia, yamesema yameteka ngome ya mwisho ya wanamgambo wa Kiislamu kusini mwa nchi hiyo.

Msemaji wa serikali amesema majeshi yamekiteka kijiji cha pwani cha Ras Kamboni ambako wanamgambo wa Kiislamu walikimbilia.

Taarifa zinasema wanamgambo wengi wamekamatwa.