1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU: Mapambano nchini Somalia yasababisha wasi wasi

9 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCks

Kwa siku ya pili kwa mfululizo,vikosi vya serikali ya mpito ya Somalia vikisaidiwa na majeshi ya Kiethiopia vimepambana na wanamgambo wa Muungano wa Mahakama za Kiislamu,kusini magharibi mwa nchi.Afisa wa Mahakama za Kiislamu, Mohamed Ibrahim Bilal amesema,vikosi vya serikali vilishambulia kijiji cha Ramáddey,kilicho kama kilomita 80 kusini-magharibi ya mji wa Baidoa ambako serikali ya mpito ina makao yake.Lakini waziri mkuu Ali Mohamed Geddi alisema,wanamgambo wa Muungano wa Kiislamu,ndio walioshambulia vituo vya serikali.Wakati huo huo,wakazi wa Baidoa wamesema,tangu siku mbili za nyuma,harakati za kijeshi zimezidi katika mji huo,hali ambayo inazusha wasi wasi wa vita kuripuka upya katika Pembe ya Afrika.