1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU : Meli ya kivita ya Marekani yashambulia Somali

3 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBvS

Meli ya kivita ya Marekani imeshambulia kwa makombora maeneo yanayotuhumiwa kuwa ya Al Qaeda kaskazini mashariki mwa Somalia baada wapiganaji wa Kiislam kupambana na wanajeshi wa jimbo la Puntland lenye mamlaka fulani ya kujitawala.

Wanamgambo wanane wa kigeni waliuwawa kwenye mapambano hayo.

Maafisa wamesema Meli ya kivita ya Marekani ya US Destroyer imeshambulia maeneo kadhaa wakati wa usiku ambapo wanamgambo wa Kiislam inaaminika kuwa wana kambi zao kwenye milima ilioko mbali kabisa nje ya mji wa mwambao wa Bargal.

Wizara ya Ulinzi ya Marekani imekataa kuthibitisha shambulio la0 hilo lakini imeapa kuendelea kuwaandama Waislamu wa siasa kali.