1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU: Mkutano wa Somalia umeahirishwa hadi Alkhamisi

15 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBiV

Mizinga ya bomu imevurumishwa kwenye sherehe ya kufungua mkutano wa amani wa Somalia mjini Mogadishu,lakini imekosea jengo linalolindwa vikali.Inadhaniwa kuwa shambulizi hilo limefanywa na waasi wa kundi la Kiislamu.Rais Abdullahi Yusuf alikuwa akihotubia mamia ya viongozi wa makundi ya kikabila,wanasiasa pamoja na wababe wa vita wa zamani,makombora hayo yalipoanguka karibu na eneo hilo.Wanamgambo wa Kiislamu wamekula kiapo kushambulia mkutano ulioahirishwa hadi siku ya Alkhamisi,wakati wajumbe wengine wakingojewa kuwasili mjini Mogadishu.Takriban wajumbe 1,350 kutoka kila pembe ya Somalia wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo,unaotazamwa kamani nafasi ya mwisho kwa serikali ya mpito,kuleta amani nchini Somalia na kuumaliza mgogoro pamoja na wanamgambo wenye itikadi kali za Kiislamu.