1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU: Mripuko Somalia umeua watoto watano

7 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBl9

Si chini ya watoto 5 wa kiume wameuawa na 7 wengine wamejeruhiwa,baada ya bomu lililokuwa kando ya barabara kuripuka katika mji mkuu wa Somalia,Mogadishu.Mashahidi wamesema watoto hao walikuwa wakicheza mpira,mripuko huo ulipotokea. Inasemekana kuwa hilo lilikuwa bomu lililofukiwa ardhini.Mji mkuu wa Somalia unashuhudia miripuko ya aina hiyo na mashambulizi ya gruneti na risasi tangu vikosi vya Somalia kudhibiti mji huo katika mwezi wa Aprili.Vikosi hivyo vikisaidiwa na majeshi ya Ethiopia viliwatimua Mogadishu, wanamgambo wa Kiislamu na wapiganaji wa makundi ya kikabila baada ya kupigana vikali kwa miezi kadhaa.