1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU: Ndege ya mizigo yatunguliwa Somalia

25 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCFe

Ndege ya mizigo ikiwa na watu 11 imetunguliwa baada ya kuondoka uwanja wa ndege wa mji mkuu wa Somalia,Mogadishu.Maafisa na mashahidi katika eneo hilo wamesema,ndege hiyo siku ya Jumamosi iliangukia viunga vya kaskazini vya Mogadishu, ikiwa imeshika moto.Wizara ya ndani ya Somalia inachunguza tukio hilo.