1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU : Ngome ya mwisho ya Waislamu yatekwa

13 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCbF

Vikosi vya serikali ya Somalia vikiungwa mkono na vile vya Ethiopia vimeteka ngome kuu ya mwisho ya wapiganaji wa Kiislam nchini Somalia baada ya mapigano ya siku tano.

Ushindi huo umetangazwa masaa machache baada ya wababe wa vita kukutana na Rais Abdulahi Yusuf na kuahidi kuwajumuisha wapiganaji wao kwenye jeshi la serikali.

Waziri wa ulinzi wa Somalia Kanali Barre Aden Shire amesema serikali imeuteka mji huo wa mwambao kusini mwa Somalia ambao unatuhumiwa kuwa ulikuwa ni maficho na kambi ya mafunzo ya kundi la Al Qaeda.

Mji wa Ras Kamboni uko kusini kabisa mwa Somalia na kama kilomita 3 tu kutoka mpaka wa Kenya.