1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mogadishu. Serikali yadai ushindi.

27 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC6a

Waziri mkuu wa Somalia amedai kushinda dhidi ya wapiganaji wa Kiislamu mjini Mogadishu. Mapigano ya siku nane ya mitaani ambayo yanaemekana kuwa mabaya zaidi katika mji huo , yamemalizika.

Wanadiplomasia wa mataifa ya magharibi walikuwa na shaka na madai hayo ya serikali ya Somalia na hali ya wakimbizi haijakuwa bora kwa mujibu wa mkuu wa uratibu wa misaada ya kiutu wa umoja wa mataifa.

John Holmes ameonya kuwa operesheni za misaada haziwafikii watu wengi wanaoihitaji nchini Somalia.

Holmes amesema umoja wa mataifa utaangalia ahadi za serikali ya Somalia z

a kutozuwia upelekaji wa misaada katika muda wa siku moja ama mbili zijazo. Waziri mkuu wa Somalia amesema kuwa zaidi ya watu 300,000 ambao wameukimbia mji wa Mogadishu sasa wanaanza kurejea.