1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU: Vikosi vya amani vyashambuliwa Somalia

8 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCLL

Ripoti zinasema watu wenye silaha wamekishambulia kikundi kipya cha wanajeshi wa amani wa Umoja wa Afrika,kilichowasili mji mkuu wa Somalia Mogadishu.Inasemekana kuwa raia mmoja aliuawa na wengi wengine walijeruhiwa katika mapambano ya risasi yaliyotokea kati ya pande hizo mbili. Shambulio hilo lilitokea muda mfupi tu baada ya ndege tano zilizokuwa na wanajeshi 700 wa Uganda na zana za kijeshi kutua kwenye uwanja wa ndege wa Mogadishu.Umoja wa Afrika unatazamia kupeleka wanajeshi 8,000 kuisaidia serikali ya Somalia kurejesha usalama nchini humo baada ya wanamgambo wa Muungano wa Mahakama ya Kiislamu kutimuliwa mwishoni mwa mwaka 2006.