1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU: Wakazi wa Mogadishu washuhudia siku ya pili ya utulivu

3 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCCu

Hali ya utulivu imeendelea kwa siku ya pili mjini Magadishu, huku wakuu wa koo kubwa ya kisomali wanakijiandaa kukutana na majeshi ya Ethiopea.

Wanadiplomasia kutoka Marekani, Ulaya na Afrika wanatarajiwa kukutana mjini Cairo chini ya mwavuli wa kundi la kimataifa linalojaribu kushawishi pande hasimu nchini Somalia kufanya mazungumzo ya maridhiano.

Baada ya siku nne za mapigano yaliyopelekea mamia kadhaa kuawa na wengine kuukimbia mji huo mkuu wa Somalia, utulivu umeleta matumaini kwa wakazi zaidi ya milioni moja wa mji huo wengi wao wakiwa wanajaribu kuukimbia.

Wanamgambo wa muungano wa mahamakama za kisomalia wamejichimbia katika viunga vya vya mji huo, ambapo mashuhuda wanasema kuwa majeshi ya Ethiopea yanayoyasaidia yale ya serikali ya mpito ya Somalia yamekuwa yakitathimini nyendo zao kwa karibu.