1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU: Wakazi waanza kurejea Mogadishu

26 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CByH

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloratibu masuala ya misaada ya kibinadamu limesema watu kiasi elfu tisini wamerejea kwenye kambi viungani mwa mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, wakati ambapo hali imetulia kwa kiasi.

Wakazi karibu laki nne walikimbia makazi yao kati ya mwezi Machi na mwezi uliopita kutokana na vita kati ya wanamgambo wa Kiislamu na majeshi ya Ethiopia yakishirikiana na vikosi vya serikali ya Somalia.

Watu elfu moja, mia sita na sabini waliuawa kwenye makabiliano hayo.

Juma lililopita serikali ya Somalia ilidai imewashinda wanamgambo hao.