1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU : Wasomali wakimbia mapigano

24 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC7m

Wasomali wanakimbia mapigano ya siku sita katika mji mkuu wa Mogadishu ambapo kundi moja la haki za binaadamu linasema vikosi vya Somalia na Ethiopia hapo jana vimeuwa watu 37 katika shambulio la kuwatokomeza waasi wa Kiislam.

Kwa mujibu wa shirika la kienyeji la Elam la Amani na Haki za Binaadamu linalofuatilia maafa ya mapigano hayo katika hospitali, kwenye familia na kuhesabu maiti zinazooza barabarani kutokana na jua idadi ya vifo kutokana na mapigano hayo ya karibuni imefikia watu 267.

Haifahamiki wanajeshi wangapi wa Ethiopia na wa serikali ya Somalia wameuwawa katika mapigano hayo.