1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU : Watu wanne wauwawa

22 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBgQ

Watu wanne wameuwawa na wengine kadhaa kujeruhiwa hapo jana katika mripuko wa bomu la mkono na mashambulizi ya risasi katika mji mkuu wa Somalia ambapo wajumbe wamekuwa kwenye mazungumzo ya amani.

Waasi walirusha bomu hilo kwenye doria ya jeshi katika soko la Bakara lilioko kusini mwa Mogadishu na kuuwa watu watatu akiwemo mwanajeshi mmoja.

Wanajeshi walifyetuwa risasi na kumuuwa raia mmoja.

Vifo hivyo vinatokea wakati wajumbe wakikutana kwa mazungumzo ya usuluhishi katika jengo la ghala la polisi lenye ulinzi mkali kaskazini mwa Mogadishu.