1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mogadishu. Watu wawili wauwawa kwa risasi.

12 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCJm

Watu wawili wameuwawa kwa risasi mjini Mogadishi nchini Somalia , baada ya watu wenye silaha kushambulia kambi ya wanajeshi wa Ethiopia. Watu walioshuhudia wanasema kuwa kijana mmoja na mwanamke mmoja wameuwawa na wengine watano wamejeruhiwa wakati majeshi ya Ethiopia yakilinda maeneo ya serikali yalipopambana na wapiganaji.

Mamia ya raia wameuwawa katika mapambano mjini Mogadishu tangu majeshi ya pamoja kati ya Ethiopia na yale ya serikali ya Somalia kuuondosha utawala wa mahakama za Kiislamu kutoka eneo la kusini mwa nchi hiyo pamoja na maeneo ya kati.

Mabaki ya kundi la Waislamu linalaumiwa kwa ghasia hizo. Somalia imekuwa bila serikali yenye mamlaka tangu kuangushwa kwa dikteta Mohamed Siad barre mwaka 1991.