1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU: Waziri Mesfin ziarani Somalia

25 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CByR
Waziri wa nje wa Ethiopia,Seyoum Mesfin amewasili mji mkuu wa Somalia,Mogadishu kwa ziara yake ya kwanza,tangu vikosi vya Ethiopia kumaliza mapigano yaliokuwa makali kabisa mjini humo. Waziri Mesfin,aliefuatana na kama maafisa 30, alipokewa na Rais Abdullahi Yusuf Ahmed na Waziri Mkuu Ali Mohamed Gedi mjini Mogadishu.Mwanzoni mwa mwaka huu,vikosi vya Ethiopia na vya Somalia viliwatimua wanamgambo wa Muungano wa Mahakama ya Kiislamu,wanaoipinga serikali ya mpito ya Somalia iliyoundwa mwaka 2004