1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU:Mapigano makali yaendelea Somalia

22 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCGZ

Vifaru vya majeshi ya Ethiopea yanayolinda makao makuu wa serikali ya mpito ya Somalia, vimepambana na wanamgambo wa kisomali waliyoshambulia makao hayo.

Hata hivyo mpaka sasa hakuna idadi rasmi ya watu waliyokuawa.Lakini kwa mujibu wa kituo cha television cha CNN kiasi cha watu 22 wameuawa katika mapigano hayo.

Wadadisi wanaashiria itakua vigumu kuidhibiti hali aya mambo bila ya kuwasili idadi inayohitajika ya wanajeshi wa kikosi cha kulinda amani cha umoja wa Afrika.

Wakati huo huo kuna taarifa za kulipuka kwa mapigano huko kwenye mji wa Ramadhani kaskazini mwa Mogadishu, ambapo mamia ya watu, wengi wakiwa ni watoto na wanawake wameonekana wakiuhama mji huo kuyakimbia mapigano, wakitumia punda.

Wanamgambo wa muungano wa mahakama za kiislam wameapa kupigana dhidi ya majeshi ya serikali yanayoungwa mkono na jumuiya kimataifa.

Hapo jana watu wanaoaminika kuwa ni wanamgambo wa kisomali, waliuburura mwili wa askari jeshi la serikali katika mitaa ya Mogadishu, kabla ya kuuchoma moto.