1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU:Viongozi wa Somalia kuzuru Saudia

25 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Cs

Mfalme Abdulla wa Saudia amewaalika nchini mwake viongozi wa ngazi za juu wa serikali ya Somalia ikiwa ni juhudi za kuwapatanisha kufuatia mvutano wa kisiasa uliokwamisha shughuli za serikali.Rais Abdullahi Yusuf Ahmed anashinikiza bunge kumuondoa madarakani Waziri Mkuu Ali Mohamed Gedi kwa madai kuwa kushindwa kutimiza majukumu yake ya kumaliza ghasia zinaziosababishwa na wanamgambo mjini Mogadishu,kuunda katiba mpya aidha kuundaa serikali ya shirikisho.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo Bwana Gedi anatarajiwa kufunga safari yake ya Saudia akitokea Ethiopia anakofanya mazungumzo na maafisa wa serikali na wanadiplomasia wa kigeni.Majeshi ya Ethiopia yanaunga mkono serikali yake japo makao makuu ya Umoja wa Afrika yako mjini Addis Ababa nchini humo.

Viongozi hao watatu walitiliana saini makubaliano ya maridhiano mjini Jeddah nchini Saudia kufuatia mazungumzo ya amani yaliyokwama yaliyofanyika mjini Mogadishu.Wawakilishi wa vyama vya upinzani walisusia kikao hicho cha mwezi Agosti kilichosababisha wanadiplomasia kutoa wito wa kuwa na mpango wa kuwashirikisha wahusika wote ili kujaribu kumaliza mgogoro wa Somalia.

Haijulikani iwapo Bwnaa Yusuf na Spika wa bunge Aden Mohamed Nur ambaye ni mbabe wa kivita wa zamani ameridhia mualiko huo.Wabunge wa serikali ya muda ya Somalia walioko mjini Baidoa walishindwa kuanzisha majadiliano kuhusu hatma ya Bwana Gedi,.