1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU:Wanamgambo 16 wa Shabab wakamatwa Mogadishu

10 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBt0

Polisi nchini Somalia imesema watu 16 wanachama wa kundi la wanamgambo la Shabab linalodaiwa kuhuusiana na mahakama za kiislamu nchini humo wamekatwa kwa tuhuma za kuhusika na uasi.

Serikali ya Somalia imekuwa ikijaribu kuwasaka wapiganaji wa mahakama za kiislamu ambao wameapa kuanzisha mapambano sawa na yale yanayoendelea Iraq hadi pale nchi hiyo itakapokuwa chini ya utawala wa kiislamu.

Kundi hilo la Shabab pamoja na mahakama za kiislamu wanadaiwa kuwa wafuasi wa mtandao wa kigaidi wa Alqaeda.

Mayor wa mji mkuu wa Somalia Mogadishu,bwana Mohammed Dheere amesema polisi wamepata silaha kadhaa katika msako huo.

Somalia imekumbwa na ghasia tangu mwaka 1991 baada ya wababe wakivita kumng’owa madarakani Dikteta Mohammed Siad Barre na baadae kupigana wenyewe kwa wenyewe.