1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU:Watu saba wameuwawa katika mlipuko wa bomu la kutegwa ardhini

24 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7D3

Watu saba wameuwawa na wengine 16 wamejeruhiwa baada ya gari lililo jaa watu walilokuwa wakisafiria kukanyaga bomu la kutegwa ardhini katika eneo la kaskazini mwa mji mkuu wa Mogadishu.

Duru za hospitali ya Keysaney zimefahamisha kuwa watu hao 16 wamelazwa katika hospitali hiyo.

Wakati huo huo serikali ya Saudi Arabia imewaalika viongozi wa serikali ya mpito ya Somalia kwenye mazungumzo ya kutafuta kutatua mzozo wa kisiasa unaowakumba viongozi wa Somalia.

Mualiko huo kwa rais Abdillahi Yusuf, waziri mkuu Ali Mohamed Gedi na spika wa bunge Sheikh Adan Madobe umekuja siku chache tu kabla ya wawakilishi wa bunge la Somalia kuanza kujadili kuhusu lini utakapomalizika muda wa miezi 30 wa uongozi wa waziri mkuu wa Somalia.