1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU:Watu watano wameuwawa mjini Mogadishu

5 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7IH

Takriban watu watano wameuwawa kufuatia kurushwa guruneti katika soko kuu la mjini Mogadishu.

Mfanyakazi katika mahakama ya mjini Mogadishu ni miongoni mwa watu waliouwawa, askari wawili wamejeruhiwa katika shambulio hilo ambalo limetokea siku moja tu baada ya serikali kutangaza kuwa itaanzisha msako mkali.

Wakati huo huo balozi wa Uganda nchini Somalia bwana Sam Turyamuhika amesema kwamba ametiliana saini makubaliano na serikali ya mpito ya Somalia ya rais Abdilahhi Yusuf ambapo Uganda itasaidia katika kutafuta maridhiano kati ya serikali na makundi ya upinzani.

Uganda ina wanajeshi wake 1800 wanaotekeleza jukumu la kulinda amani nchini Somalia.