1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Moja asilimia ya watu duniani ni tajiri mno

Sekione Kitojo
24 Januari 2018

Wahariri Ujerumani wamezungumzia kongamano la kiuchumi duniani Davos, jukumu la Martin Schulz katika serikali ya muungano ya Ujerumani, na silaha za Ujerumani, kutumika katika mapambano ya Uturuki dhidi ya Wakurdi Syria.

https://p.dw.com/p/2rQYr
Justin Trudeau World Economic Forum
Waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau akihutubia DavosPicha: picture-alliance/empics/P. Chiasson

Gazeti  la  Hannoversche Allgemeine Zeitung  la  mjini Hannover. Linazungumzia  kuhusu mkusanyiko wa  viongozi  wa kitaifa na biashara  duniani  mjini  Davos. Mhariri  anaandika  kwamba wahenga walinena  kwamba hali  bora ya kiuchumi  katika  mataifa ya  magharibi yenye viwanda  inaweza  kuwa  na  matokeo  mabaya hapo  baadaye.  Mhariri anaendelea:

Soko la  hisa  la  Dax   hapa  Ujerumani  limepanda  na  kufikia  kiasi cha  juu  kabisa, mjini  New York ,  Dow Jones  lina paa,  lakini ukilinganisha  maeneo  mengine  ya  dunia   hali  ni  ya  utegemezi  kwa  kila  kitu. Shirika  la  mpango wa  maendeleo  la  Oxfam linasema, moja  asilimia  ya  watu wote duniani  wana  utajiri mkubwa  ikilinganishwa  na  asilimia  99  ya  watu duniani. Hali  hii itaendelea  hadi  lini,?  anauliza  mhariri.

Baadhi  ya nadharia  za kale za  Karl Max , aliyezaliwa  miaka  200  iliyopita, zinaweza kuthibitishwa. Duniani  mataifa yanafaidika sana na utajiri  kwa  kufanya kazi  kidogo  tu.  Moja  kati  ya  vitu vinavyoleta  utajiri  huo  ni  kodi ya  makampuni  makubwa. Trump hivi  sasa  anaelekea  upande  mwingine, anasisitiza  zaidi  kuhusu , "Marekani kwanza", akichukua  hatua  ya  kupunguza  kodi.

Kwa upande  wa suala  la  kuunda  serikali  ya  muungano  nchini Ujerumani  kati  ya  vyama  vya kihafidhina vya CDU/CSU na  kile cha  Social Democratic cha  SPD, mhariri  wa  gazeti  la  Rhein-Zeitung  la  mjini Koblenz  anaandika.

Ama  wanachama  wa  chama  cha  SPD  wamwangushe  Schulz  na kumpa  mtu  mwingine  kiti  chake , ama wamuunge  mkono kwa dhati. Pamoja  na  hayo  kiongozi  huyo  wa  chama  anatarajiwa kuwa  naibu  kansela  katika  muungano  huo, akipata  pia  nyadhifa muhimu  katika  baraza  la  mawaziri.

Martin Schulz anaingia  katika  serikali  bila  ya  uzoefu  wowote  wa uwaziri , nafasi ya  chama  cha  SPD  bila  shaka  itakuwa dhaifu katika  serikali. Na kwa  hiyo  chama  cha  SPD hatimaye hakitakuwa  na  nafasi  nzuri ukifika  wakati  wa  uchaguzi, kwa  kuwa mkuu  wa  chama  hatakuwa  na  kazi  nyingine  tena  isipokuwa kuwatuliza  viongozi  wenzake  na  wanachama  ambao hawajiamini. Ni  kiongozi  mwenye uhakika tu na  anayejua  anafanya  nini , anaweza  kufanikiwa.

Kuhusu  mjadala juu  ya  silaha  za  Ujerumani  zinavyotumika  na jeshi  la  Uturuki  kupambana  na  Wakurdi  nchini  Syria , mhariri  wa gazeti  la  Stuttgarter Nachrichten  anaandika.

Si  muhimu  sana , iwapo  ushahidi  uliopo hivi  sasa  ni  fursa pekee, kwamba  mshirika  wa  NATO Uturuki  inatumia  silaha zilizotengenezwa  Ujerumani  katika  mapambano  yake  na Wakurdi nchini  Syria,  kuweza kuilazimisha  Ujerumani  kutoa  msimamo wake wazi. Kwa  ujumla  hali  hii  ni  suala  la  kimaadili. Mshikamano katika  NATO  ni  muhimu, kwa  kuwa  jumuiya  hiyo  inaihakikishia Ujerumani  usalama wake.  Pamoja  na  hayo  ni  muhimu  kufahamu, anaandika  mhariri  kwamba  mauzo  ya  silaha nchi  za  nje hayapaswi kuchochea  mizozo.

 

Mwandishi: Sekione  Kitojo / inlandspesse

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman