1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MORONI : Comoro yatafakari hatua ya kijeshi dhidi ya Njouan

14 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBrz

Comoro imesema hapo jana itafikiria kuchukuwa hatua za kijeshi dhidi ya kisiwa kinachoasi cha Njouan ambacho uogozi wake uliojitangazia madaraka umefanya uchaguzi kwa kuikadi jumuiya ya kimataifa halikadhalika serikali ya umoja ya visiwa vya Comoro.

Uchaguzi katika kisiwa cha Anjouan ulifanyika kama ilivyopangwa hapo Jumapili licha ya uamuzi wa serikali ya taifa ya umoja wa visiwa hivyo kuuahirisha kwa wiki moja kutokana na sababu za usalama.

Mazungumzo ya siku mbili kati ya jumuiya ya kimataifa chini ya uongozi wa Umoja wa Afrika yameshindwa kuwashawishi maafisa wa serikali ya Anjouan kufuta matokeo ya uchaguzi huo na kufanya uchaguzi mwengine Jumapili ya tarehe 17 mwezi huu.

Ibrahim Abdallah mshauri wa Rais Abdallah Sambi wa serikali kuu ya Comoro anaelezea kwa nini serikali hiyo imeamuwa kutakafakri hatua ya kijeshi dhidi ya kisiwa cha Njouan.

Njouan ilifanya uchaguzi hapo Jumapili na kumtangaza rais wake wa zamani Mohamed Bakar kuwa kiongozi wa kisiwa hicho.

Kisiwa cha Ngazija na Moheli vilifanya uchaguzi huo kama ilivyopangwa hapo Jumapili.