1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Moroni:Maandamano yaandaliwa kupinga Ufaransa kubakia Mayote.

24 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCpg

Wakaazi wa kisiwa kikuu cha Ngazija cha Umoja wa visiwa vya Komoro, wamepanga maandamano siku ya Jumapili, wakati waziri wa ushirikiano na maendeleo wa Ufaransa Bibi Brigitte Girardin atakapowasili kwa ziara rasmi visiwani humo.

Maandamano hayo ni ya kudai kurejeshwa katika mamlaka ya Komoro, kwa kisiwa cha Mayotte ambacho bado kinakaliwa na Ufaransa, tangu Comoro ilipojitangazia uhuru 1995.

Ufaransa hadi sasa imekataa kuheshimu maazimio ya Umoja wa mataifa na Umoja wa Afrika, kuitaka iheshimu matakwa ya Wakomoro.

Bibi Girardin kwa wakati huu, yuko ziarani nchini Tanzania, ambako Ufaransa imesaini makubaliano ya kuipa Tanzania Euro milioni 46, kuimarisha sekta ya utalii, maji na elimu, katika kipindi cha miaka mitano ijayo.