1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW: Boris Yelstin azikwa kwa heshima ya kitaifa

25 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC7B

Rais wa zamani wa Urusi Boris Yelstin amezikwa leo mjini Moscow kwa heshima ya kitaifa wanayopewa viongozi.

Rais huyo wa zamani aliaga dunia siku ya jumatatu akiwa na umri wa miaka 76 kutokana na ugonjwa wa moyo.

Ibada ya wafu ilifanyika katika kanisa katoliki la kristo mwokozi ambalo Boris Yelstin alisaidia kulijenga upya baada ya kanisa hilo kubomolewa chini ya utawala wa Kisovieti.

Miongoni mwa waombolezaji waliotoa heshima zao za mwisho ni pamoja na rais Vladmir Puttin wa Urusi, rais wa zamani wa Urusi Mikhail Gorbachev na wageni wengine mashuhuri kutoka pembe zote za dunia wakiwemo rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton na George Bush baba yake rais wa Marekani George W Bush, rais Horst Köhler wa Ujerumani pia ni miongoni mwa viongozi waliohudhuria maziko hayo.

Katika hotuba yake rais Vladmir Puttin wa Urusi alisema.

Mtu aliyetuletea enzi mpya ametupa kisogo. Yeye ndie aliyesababisha kuibuka Urusi ya kidemokrasia, huru na Urusi iliyoacha milango wazi kwa dunia na ambako madaraka kweli yanadhibitiwa na wananchi.